Kuna baadhi ya watu hasa vijana ambao wamekuwa wao kutwa kucha ni kuhangaika kwenye mitandao, ‘INTANETI’ wakitafuta njia ama mitandao wanayodai ni ya kuwaunganisha na taasisi au vyama vitakavyowasaidia kupata utajiri wa haraka au haramu. Wanapokutana na tovuti kama hizi za kwetu zilizokuwa na majina au kaulimbiu zenye hisia za utajiri au pesa, basi pasipo hata kusoma makala hizo kama ndani zinazungumzia kitu gani wao moja kwa moja huhisi wameshakutana na kile walichokuwa wakikitafuta, mara moja huanza kupiga simu wakiulizia jinsi ya kujiunga na mtandao wanaodhani unagawa utajiri.
Mgunduzi wa INTANETI Sir Tim Berners Lee hapo mwaka 1989.
Tunapenda kuwashauri na kuwaeleza ukweli kwamba, kwanza mtandao wa Intaneti watu waliouasisi akiwemo mgunduzi mwenyewe Sir Berners Lee mwaka 1989, hata na akina Steve Jobs mgunduzi wa kompyuta hizi za mezani tunazotumia leo miaka ya 70 pamoja na smart phones, Bilionea Bill Gates mzee wa software aliyeanza tangu miaka hiyo ya 70 pamoja na ‘Bwanamdogo’ Mark Zurkerberg aliyeasisi FACE BOOK juzijuzi mwaka 2004, wote hawa hawakuwa na lengo la intaneti itumike kwa malengo haramu au ya kuleta uharibifu, intaneti ililetwa kumkomboa binadamu, kumpa uhuru ikiwa ni pamoja na kuwaondolea wanyonge hali ya kutokuwa na haki ya kupata taarifa na kuondokana na minyororo ya umasikini.
Mwanzilishi wa kampuni ya Apple komputa za mezani, na smartphones, Hayati Steve job.
Uliwahi kusikia skendo za akiina Edward Snoden na Julian Assange wa Wikileaks, na Marekani taifa kubwa lilipotaka kuutumia mtandao wa intaneti na teknolojia ya habari kukandamiza haki za watu wakawaida, uliona ilivyopigiwa kelele na wanateknolojia, wagunduzi wenyewe na wapenda haki duniani? Hivyo nataka utambue jinsi ambavyo intaneti isivyopaswa kutumiwa kwa maswala ambayo hayana maadili wala kumjali binadamu wa kawaida. Tena waasisi hao waliofanya kazi ngumu usiku na mchana wakivuja jasho ili kuvumbua teknolojia ya kumkomboa mwanadamu wangekusikia ukisema unataka utumie intaneti kwa malengo hasi ya kutaka kutajirika kimiujiza pasipo kufanya kazi wangekushangaa sana.
Mwanzilishi wa mtandao maarufu wa facebook Mark Zuck.
Uchawi, nguvu za giza, dhana potofu, chuki, uvunjivu wa haki za binadamu, kueneza hofu, wizi, unyanganyi, ulaghai, uwongo, ama ubaguzi wa aina yeyote ule wa binadamu iwe ni kikabila, dini au rangi hauna nafasi kabisa kwenye mtandao wa intaneti. Kama huamini haya ninayoyasema ukidhani intaneti ni kichaka cha wahalifu au watenda maovu basi hebu anzisha blogu, au website yeyote ile kisha uanze kuhubiri chuki, au mambo ambayo yanaingilia uhuru wa watu wengine tuone kama utakaa hewani hata miezi 2.
Julian Assange kushoto na Edward Snowden kulia.
Kwa hiyo ukisikia kuna mtandao au tovuti inayoweza kumpa mtu utajiri kwa njia za kimiujiza usikubali, kataa, hizo ni “scams” utapeli. Utajiri unakuja baada ya mtu kufanya kazi halali akizingatia kanuni zote za ujasiriamali na wala hakuna utajiri unaoweza kupatikana ndani ya kipindi kifupi kama mwezi mmoja miwili au hata mwaka, labda iwe umeshinda bahati na sibu au umerithi mali za wazazi wako baada ya Mungu kuwachukua. Unaweza kutajirika kwa kuweka malengo na mipango ya muda mfupi na mrefu. Kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA kimeelezea vizuri sana namna unavyoweza ukajiwekea malengo yako ya kiuchumi na kimaisha kwa ujumla.
- See more at: http://www.jifunzeujasiriamali.com/utajiriwamiujiza.html#sthash.2DiTNG4k.dpuf