Lil Wayne mnamo 2011
Maelezo ya awaliAmezaliwa27 Septemba 1982(umri 34)Asili yakeNew Orleans, Louisiana, United StatesAina ya muzikiHip hopKazi yakeRapa, Mwigizaji, CEO, Msanifu[1]AlaSautiMiaka ya kazi1993–mpaka sasaStudioCash Money, Young Money, UniversalAme/Wameshirikiana naHot Boys, Birdman, T-Pain, Drake, Young Money, Kanye West, Young Jeezy, DJ Khaled, Mack Maine, Rick RossTovutiwww.lilwayne-online.com
Dwayne Michael Carter, Jr. (amezaliwa tar. 27 Septemba 1982) ni mshindi wa Tuzo za Grammy - akiwa kama rapa wa muziki wa hip hop bora kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lil Wayne. Alijiunga na studio ya Cash Money Records akiwa bado yungali bwana mdogo na akabahatika kufanya rekodi kadhaa katika studio hiyo. Wayne alikuwa mmoja kati ya waliokuwa wanachama wa kikundi cha muziki wa rap cha Hot Boys.
Maisha ya awali
Alizaliwa kama Dwayne Michael Carter, Jr. na kukulia mjini Hollygrove karibu kidogo na mji wa New Orleans, Louisiana. Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, akakutana na Bryan Williams, rapa na ndiyo mmiliki wa studio ya Cash Money Records. Baada ya makutano hayo, Wayne akarekodi rap flani ya michano katika studio hiyo ya Williams kwa kutumia chombo maalum cha kuweza kukujibu wakati unachana. Na kwa bahati nzuri michano hiyo ilimwacha hoi mmiliki huyo wa studio na kuthubutu hata kumwingiza Wayne katika studio yake. Wayne pia ana mtoto wa kike mmoja aitwaye Reginae Carter, aliyezaa na Bi. Antonia "Toya" Johnson, demu wake wa kitambo toka shule. Wawili hao walikuja kuoana wakati ule wa Siku Kuu ya Wapendanao ya mwaka wa 2004, lakini wawili hao walikuja kutarikiana mnamo mwaka wa 2006.
Albamu za Lil Wayne
- 1999: Tha Block Is Hot
- 2000: Lights Out
- 2002: 500 Degreez
- 2004: Tha Carter
- 2005: Tha Carter II
- 2008: Tha Carter III
- EP albums
And
- 2007: The Leak