Rapa Young Thug amehojiwa na jarida la The Guardian,kuhusu mambo tofauti ambayo maadui wake hutumia kumponda na kumuongelea vibaya.
Young Thug kaulizwa kuhusu kuvalia nguo za kike na kama anapendelea kuwa na wanaume au wanawake?
Young Thug anasema “Napenda kuvaa nguo za kike kwa sababu zinanikaa vizuri zaidi, nguo za kike zinakuja kwenye size ile nayoitaka na hata jeans nazovaa ni za kike tu, Jeans nazovaa zote ni za kike hata hii niliyovaa hapa na kama kuna kitu cha kiume kwenye kabati langu basi itakuwa t shirt na sneaker tu, asilimia 90 ni mavazi ya kike“
Kuhusu mahusiano na jinsi gani anapendelea ,Young alikwepa swali hilo.
