Skip to main content

Sakata la Nape: Raisi hakuwa na sababu ya kupanic

Mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri aliyofanya Rais jana hayakuwa na uharaka wowote, badala ya kuonekana ni mabadiliko ya kawaida yameonekana kama yamefanywa kuonyesha yeye ni nani. Zaidi yamemchora rais kama ni mtu wa aina gani, mtu wa jazba, asiye na ustahimilivu, mtu mwenye pupa, anayelipiza kisasi na mwenye upendeleo fulani.

Baada ya Nape kupokea ripoti ya tume aliyounda hata kama Rais hakufurahishwa alitakiwa kwanza kutulia, kwa vile ripoti ilikuwa ipelekwe kwake alikuwa na uwezo wa kuonyesha hisia zake kwa kuitupilia mbali kuliko kuonyesha hisia zake kwa kumtumbua Nape ndani ya masaa 12 baada ya ripoti kukabidhiwa.

Kitu kingine ambacho rais angefanya bila kuonyesha chuki kwa mtu mmoja, angesubiri muda aliopanga kufanya mabadiliko ya jumla kwenye baadhi ya wizara kama tulivyokuwa tunatarajia na kumtoa mtu asiyemtaka, lakini kubadili baraza ghafula kwa ajili ya mtu mmoja na wengine kuteuliwa pengine kabla ya kuapishwa kuwa wabunge kamili kinachukuliwa kama kitendo cha ku panic, na kiongozi mkubwa namna hii hatakiwi kutenda mambo wakati akiwa na ghadhabu.

Popular posts from this blog

MAPENZI NI NINI?: Jua maana ya mapenzi

SOCIAL HALL    Upendo umetokana na neno la kigiriki “ahab aheb” lenye maana hisia kali na muhathirika wa ndani. Upendo ni hisia kali, upendo chimbuko lake ni moyoni upendo ni Mungu ameuweka ndani ya moyo wa mwanadamu, upendo ni maisha ya mtu na ni utaratibu wa mtu hivyo mtu anapo amua kumpenda mtu mwingine mtu huyu anakua ameamua kuhatarisha maisha yake kwa mtu Fulani. Ameamua kuuweka moyo wake kwa mtu Fulani. Ameathirika ndani ya moyo wake kwa ajili ya mtu Fulani akili ambayo ndio chanzo cha mapenzi imekubaliana nayo. Najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni akili,kama akili ikichoka hakuna mapenzi hivyo ndio maana hata maandiko yanasema “ Ishini na wake zenu kwa akili”   Maana mapenzi la kweli yanahitaji akili timamu uwe na muda wa kufikiri kabla ujafanya lolote. Kuishi na mtu kunahitaji akili timamu, sasa mtu huyu amefanya maamuzi ya kiakili, kimwili na kiroho kuwa wewe unamfaa hivyo unatakiwa kuyaheshimu...

Historia ya Lil wayne

Lil Wayne Lil Wayne mnamo 2011 Maelezo ya awaliAmezaliwa 27 Septemba   1982 (umri 34)Asili yake New Orleans, Louisiana ,  United States Aina ya muziki Hip hop Kazi yake Rapa ,  Mwigizaji ,  CEO ,  Msanifu [1] Ala Sauti Miaka ya kazi1993–mpaka sasa Studio Cash Money ,  Young Money ,  Universal Ame/Wameshirikiana na Hot Boys ,  Birdman ,  T-Pain ,  Drake ,  Young Money ,  Kanye West ,  Young Jeezy ,  DJ Khaled ,  Mack Maine ,  Rick Ross Tovuti www.lilwayne-online.com Dwayne Michael Carter, Jr.  (amezaliwa tar.  27 Septemba   1982 ) ni mshindi wa  Tuzo za Grammy  - akiwa kama rapa wa muziki wa hip hop bora kutoka nchini  Marekani . Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama  Lil Wayne . Alijiunga na studio ya  Cash Money Records  akiwa bado yungali bwana mdogo na akabahatika kufanya rekodi kadhaa katika studio hiyo. Wayne alikuwa mmoja kati ya waliokuwa ...

Freemason na familia 13 za Illuminant

FREEMASONS NA FAMILIA 13 ZA ILUMINATI NI chama cha Prieure de Sion (Priory de Sion) kilichoanzishwa na familia ya 11 ya Illuminati inayoitwa Freeman Illuminati bloodlines ndicho kilichosababisha kuanzishwa kwa ‘Uprotestant’ au ‘Upinzani’ ndani ya dini. Wakainuka mashujaa wengi waliopinga mafundisho machafu yaliyoingizwa ndani ya imani ya kweli ili kutetea neno la Mungu litawale tofauti na mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Miongoni mwa mashujaa walioinuka kupingana na mafundisho ya chama cha Prieure de Sion alikuwa Martin Luther. Kumbuka kwamba wapinzani ‘Protestants’hawa walikuwa wanapinga mafundisho wakiwa ndani ya mifumo ya dini zao. Hata hivyo hawakufanikiwa kuleta matokeo mazuri ya upinzani wao na hivyo wakaamua kutoka na kujitenga na dini wakiwa na baadhi ya mafundisho machafu waliyoyarithi kutoka kwenye mifumo potofu ya kidini. Wakiwa wamejitenga, sasa waliamua kufanya ‘matengenezo’ kwa lengo la kuondoa mafundisho machafu na ku...