Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda.Na. Dorcas Safiel, Alex Sonna.
Hii ni historia ya muheshimiwa paul makonda mkuu wa mkoa jijini Dar es salaam, amezaliwa tarehe 15\2\1982 huko Kolomije wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza katika zahanati ya Kolomije siku ya Jumatatu saa 1;30 Asubuhi ni mtoto wa kipekee wa kiume katika familia ya mzee Makonda na bi.Suzan
mh.Paul Makonda ametoka kwenye familia ya kawaida mama yake alisoma mpaka darasa la 7 na baba yake hakusoma kabisa lakini pia alihishi katika kusudi la mungu na kumtumikia pia ni kitu kilichomfanya awe bora katika ukuaji wake wakati wote, alibahatika kuwa na ndugu wa kike lakini aliweza kuishi ndani ya mwaka na nusu toka kuzaliwa kwake na kufariki dunia.
Amesoma shule ya msingi katika shule ya kolomije,sekondari alisoma kutokana na changamoto za kipato katika familia hakuweza kwenda kidato cha tano na kwenda chuo Mbegani chuo cha uvuvi mjini bagamoyo kuanza ngazi ya cheti,diploma na ata kufika chuo kikuu katika kuchukua shahada yake sifa kubwa aliyokuwa nayo chuoni na aliyoacha hapo wanafunzi wengi kubadilika tabia na kumtumikia mungu, Pia nyumbani alikuwa mchapakazi asiye mvivu alikuwa radhi kukaa njaa lakini kufanya kazi daima hasa katika kulima alimpa mama yake faraja pale alipokuwa na huzuni, lakini msikivu kwa kila mtu amekuwa faraja katika familia ya makonda wakati wote katika maisha yake hakuwayi kufikiri kama kuna mtu atamfanyia mahamuzi zaidi yake mwenyewe. Mh.Paul Makonda ametia maisha magumu ili tu aweze kupata shahada moja alikuwa utingo wa kubeba mizigo ya watu huko mkoani Mwanza,mwaka 2001-2002 alikuwa mchimba mchanga na mkata mkaa huko Mbezi Luis pia amewayi kuwa waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Muccobs.
Mh. Paul Makonda akiwa katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015
Ni mwana siasa kupitia chama cha mapinduzi( CCM) kabla ya kuwa mkuu wa wilaya aliwayi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa ccm( uvccm) uhamasishaji na chipukizi, wakati wa Rais mstaafu dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya mkoani Dar es salaam mnamo tarehe 18|2|2015 jambo ambalo alifurahi sana na kwenda kumshukuru Mungu, changamoto ambazo aliwayi kupitia ni kama zifuatazo.
changamoto ya muda kwake ilikuwa ni kubwa sana kwani alitamani yawe masaa48 ili aweze kufanya kazi zake vizuri.changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo ilimpelekea kutoa 75% kuwalipa wanasheria kwa ajili ya kutatua migogoro hiyo.ufisadi uliokithirirushwauchafu wa mazingira wilaya ya kinondonihuduma za afya na elimu.Hata hivyo tarehe 13\3\2016 Rais wa muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuri aliweza kumteuwa kuwa mkuu wa mkoa wa jiji la Dar es salaam katika sekta ya kuwa mkuu wa mkoa alikuta changamoto zifuatazo;
omba omba jijini Dar es salaam ambao walikuwa chanzo cha uchafu wa jiji na kufanyika kwa uharifu na kushuka kwa elimu.madawati shuleniupungufu wa shule za sekondari za serikali.uchafu uliokithiri jijini Dar es salaam wasichana wanao jiuza miili yao.utumiaji mbaya wa sehemu za starehe.Mh,Paul makonda kwanza ni kijana mdogo katika siasa na pia mkakamavu kwani mtu yeyote anaweza kujifunza kupitia kwake kuhusu maisha lakini pia haya ni mambo 8 usiyo yajua juu ya Mh.Paul Makonda katika kupenda kazi yake pamoja na nchi yake ya Tanzania..
28\2\2016 Mkuu wa wilaya ya kinondoni Paul Makonda aliaza kupiga hatua ya kuwapigania walimu ili waweze kusafiri bure ikiwa kama jukumu lake la kusaidia kutekeleza lengo la Rais dkt.John Pombe Magufuri kuboresha sekta ya elimu. 16\2\2016 Mh.Paul Makonda aliaza mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira katika wilaya yake kwa kuanzisha mashindano ya vijana kwa jina la kinondoni talent search .8\3\2016 Aliazisha mkakati wa maalum wa kuanzisha mtaa maalum utakaokuwa ukihusika na biashara ya vinywaji vikali na baridi kama bar. 20\3\2016 Alitoa rai kwa watu wanaotumia silaha kinyume na sheria kwenda kuzisalimisha katika kituo cha polisi lakini hakuishia hapo aliahidi kutoa kitika cha shilingi million moja kwa yule atakayetii agizo hilo na kuahidi kutochukuliwa hatua yeyote.10\5\2016 Katika sakata la sukari nchini Tanzania alikuwa kiongozi mnzuri wa kukamata tani 4 za sukari zilizofichwa wilaya ya kinondoni.9\5\2016Katika suala la kutumbua majipu ya watumishi hewa seikalini bado alikuwa vinzuri kwa kumsimamisha Afisa utumishi wa wilaya ya ilala baada ya kushindwa kubaini wafanyakazi hewa 11 waliokuwa wilaya hiyo. 11\4\2016 mkakati wa kuanza kupamba na omba omba kando ya barabara jijini dar uliaza April 18\4\2016 ambao waliotolewa katika maeneo ya barabara ili kupumguza uhalifu,na kufanya waweze kurudi makwao kujishughulisha.
30\4\2016 Alizindua kampeni ya usafi mkoani Dar es salaam iliyofanyika katika viwanja vya Leaders Clubs na kauli mbiu ilikuwa "usijifanye mstaarabu kuwa mstaarabu" kwa lengo la kuboresha hali ya usafi katika mitaa mbali mbali pamoja na jiji la Dar es salaam kwa ujumla.Hayo ni baadhi kati ya mengi aliyoyafanya Mh.Paul Makonda katika jiji la Dar es salaam akionyesha kukubali kufanya yote ambayo ni kero jijini hapa ndani ya miaka 5 na mengine mengi ambayo yapo njiani kuja.