Wanaume wengi wanatumia kigezo hiki kama kuthibitisha au kudhihirisha mapenzi ya dhati. Utamsikia mwingine anasema: “Sasa kama hutaki kufanya mapenzi na mimi, utakuwa hunipendi.” Kwa sababu wanawake nao wanaogopa kuachwa au wanatamani ndoa, kwa kuamini kwamba tendo hilo ni kila kitu wanajikuta wakikubali; sasa hapo inategemea, mwisho unaweza kuwa mzuri au mbaya! MAPENZI NI NINI HASA? Kila mmoja anaweza kuwa na maana yake, lakini kimsingi mapenzi hayana maana ya moja kwa moja! Kwa ujumla mapenzi ni hisia zenye msisimko wa pendo la dhati zinazotoka moyoni mwa mmoja kwenda kwa mwingine. Pendo hukamilika ikiwa wawili hao kwa wakati mmoja watahisi hisia hizo, ingawa wakati mwingine mmoja ndiyo huwa wa kwanza kuanza kuhisi hisia hizo. Tafsiri hii nimewahi kuitaja mara kadhaa katika makala zangu, kama wewe ni mdau wa kona hii utakuwa unakumbuka, kama ndiyo kwanza unasoma hapa, basi si vibaya maana utakuwa umeingiza kitu kichwani mwako. Wakati mwingine inawezekana mkajikuta mm...